Wema Aanza Kufanya Projects Kubwa Nje ya Nchi

Leave a Comment
Makundi ya mashabiki mitandaoni maarufu kama Team yamekuwa ni sehemu ya maisha ya mtandaoni ya wasanii na watu maarufu wengi hapa nchini. Linapokuja swala ya ushabiki na mada nzito team hizi huvutana kwa kutupiana maneno na wakati mwingine hadi maneno makali.
Siku za hivi karibuni baada ya mwigizaji Wema Sepetu alipoachana na mpenzi wake Shape Platnum, na badaye Shape kuamua kutoka na mwanamama Zari kutoka nchini Uganda, Mashabiki (Team) wa Shape na wale wanaomponda Wema Sepetu wamekuwa kwakiasi kikubwa wakiwatupia maneno na vijembe wale mashabiki wa Wema (Team wema), kwa picha na maneno.kiasi ambacho Team wema kuonekana kama” lossers”.

Lakini leo hii upepo umebadilika huko mitandaoni na Team wema wanaonekana kuwa na nguvu zaidi, baada ya mwigizaji Wema Sepetu kuachia baadhi ya picha akiwa nchini Ghana akifanya kazi na Van vicker ambae ni msanii mkubwa hapa Afrika.

Team wema wamepongeza sana juhudi za mwigizaji huyo kutaka kuivusha tasnia ya filamu hapa nchini na kuipeleka kimataifa hivyo wanataka Le Projectii iemdelee tunampongeza na kumpa moyo katika juhudi zake hizi za kukuza tasnia yetu.
Next PostNewer Post Previous PostOlder Post Home

0 comments:

Post a Comment