Lulu Ataja Sababu ya Kupenda Kutoka na Wanaume Waliomzidi Umri

Leave a Comment
Staa wa Filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekili kupenda kuwa na mahusiano wa kimapenzi na wanaume waliomzidi umri.

Lulu Alizungumza hayo wakati akihojiwa kwenye kipindi cha 'The Sporah Show', Lulu amezitaja sababu za kupendelea kutoka na wanaume waliomzidi umri.
SPORAH: Watu wanahisi kwamba Lulu anapenda sana kutembea na watu waliomzidi umri sana.

LULU: That’s true, sio uongo, sio sana, Napenda kudate mtu ambaye anayeweza kusimama kama mpenzi, kama kaka, kama baba, kama kiongozi. Sitakuwa tayari kuwa na ile relation leo tumeamka na Maisha Club, kesho tumeamka na Billicanas, kesho tumeamka pale tunakula chips, I need to gain from you, nje ya upenzi unanifundisha nini kwa sababu haimaanishi kwamba mi ntaishi na wewe milele, itafikia siku labda we utaondoka au mi ntaondoka, we ukiondoka mi nikibaki nimejifunza nini kutoka kwako na ntaendelea kuishi vipi.”

“Haimaanishi kwamba napenda kutembea na watu walionizidi umri labda miaka hamsini, napenda kuwa na mtu ambaye angalau ananizidi umri, anauzoefu zaidi yangu, amepitia vitu vingi, anajua vitu vingi kwamba i’ll be there as a girlfriend lakini nakuwa naiba iba kidogo […] na vitu vingine vya kitoto kitoto vingi vinakuwa hamna.” alisema Lulu.
Next PostNewer Post Previous PostOlder Post Home

0 comments:

Post a Comment