Huyu ndio kigogo mpya anaye toka na jack wolper

Leave a Comment
Achana na kina pedeshee Mangi, Dallas na Gee Modal, kigogo mpya wa staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe safari hii amenaswa laivu wakijiachia kwa raha zao.

Kwa mujibu wa chanzo, kigogo huyo ni mtu mwenye fedha zake aitwaye Jimmy Mgaya ambaye ni Mbongo mfanyabiashara aishie nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.

Chanzo hicho kilishusha data kuwa jamaa huyo ndiye aliyempangia Wolper nyumba ya kifahari iliyopo ushuani Mbezi-Beach jijini Dar.Huku akirusha picha za kimahaba za wawili hao, sosi wetu huyo alisema kuwa Jimmy ni ‘mtu f’lani hivi amazing’ kwa sababu anakata mkwanja kinoma.

Chanzo hicho kilidai kwamba picha za wawili hao wakijiachia zilipigwa maskani kwa jamaa huyo huko Durban kwenye Jimbo la KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini.

Baada ya jitihada za kumsaka mwanaume huyo kugonga mwamba, Wolper alipigiwa simu na kusomewa mashitaka yake juu ya mwanaume huyo ambapo mbali na kukiri kumfahamu Jimmy, alikuwa na haya ya kusema:

“Ni kweli namfahamu Jimmy, nilikutana naye kwenye mizunguko yangu nje ya nchi. Si kweli kwamba ni bwana’ngu. Kuhusu picha, nilipiga naye kama rafiki tu na sioni kama ni picha mbaya.”

Hivi karibuni Wolper alikiri kuwa na mwanaume lakini akawa anaogopa kumwanika kwa kuogopa kuporwa na wasichana wa mjini hivyo inaaminika ndiye huyo Jimmy.
Next PostNewer Post Previous PostOlder Post Home

0 comments:

Post a Comment