VENGU MZIMA HAJAFA-JOTI

Leave a Comment
UVUMI uliozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa mwigizaji wa kundi la Orijino Komedi Joseph Shamba ‘Vengu’ kuwa amefariki hazina ukweli wowote na zimeleta usumbufu kwa ndugu na jamaa wa msanii huyo ambaye ni mzima wa afya akiwa yupo kwake, amedhibitisha msanii mwezake Joti.

“Hatujui watu hawa wana nia gani na mwezetu, ni mtu kajisikia tu kuposti ujinga aliofikiria kama unaweza kumpatia kiki labda kwa akili yake, toka asubuhi leo simu ni nyingi sana kila mtu akikupigia na swali hilo hilo Vengu kafa?,”anasema Joti.

Msanii huyo anashauri watu kuachana na tabia ya kuchukua majukumu ya familia kutangaza mambo ya kifamilia kwani habari si lazima iwe kifo tu, habari zipo nyingi, hivyo anawaambia wapenzi wa Orijino Komedi msanii wao yu mzima wala wasidanganywe na mtu.

“Kwa kupenda kuongea uongo unaweza kuua kwa ujinga na utumiaji wa mitandao ya kijamii vibaya, tuachane na tabia za kidaku, suala la kifo lipo tu,”
Next PostNewer Post Previous PostOlder Post Home

0 comments:

Post a Comment