Anthony Martial atua Manchester United kwa pauni milioni 36

Leave a Comment
Mshambuliaji kinda wa Monaco Anthony Martial amepewa ruhusa na Shirikisho la Soka la Ufaransa kuachana na majukumu ya mechi za kimataifa na kwenda England kukamilisha usajili wake Manchester United. Dili hilo la pauni milioni 36 ambalo ukichanganya na marupurupu litafika pauni milioni 58, litamshuhudia kinda huyo wa miaka 19 akipishana na Javier Hernandez aliyeuzwa Bayer Leverkusen kwa pauni milioni 12.

Taarifa ya Shirikisho la Soka la Ufaransa limesema: "Anthony Martial aliomba ruhusa kwa kocha wa timu ya taifa Didier Deschamps ili aende England kusaini mkataba na Manchester United. "Kocha alimpa ruhusa na akaondoka kwenye kambi ya timu ya taifa saa 6 mchana na atarejea Jumanne."

Martial atakuwa kinda ghali zaidi katika historia, akivunja rekodi iliyowekwa na Manchester United wakati wanamnunua beki Luke Shaw. Ataunda 'Top Three' ya makinda ghali iliyowekwa na Manchester United hiyo ikiwa ni pamoja na Wayne Rooney aliyesajiliwa na kwa pauni milioni 30 miaka 11 iliyopita.

kinda Anthony Martial ameigharimu Manchester United pauni milioni 36
Anthony Martial (kulia) anatarajia kujiunga na Manchester United kabla dirisha halijafungwa

Previous PostOlder Post Home

0 comments:

Post a Comment