Taarifa kamili kuhusu Kajala kupigwa chupa

Leave a Comment
 Kajala akionekana na jeraha juu ya jicho lake la  kushoto kwenye shindano la vipaji Kinondoni Dar es salaam.
May 10 2015 mwigizaji wa bongomovie Kajala alikwenda kumsupport msanii Mabeste ambaye alifanya show New Maisha Club kwa ajili ya kuchangisha pesa za kumsaidia mke wake kwenye matibabu.

Kajala anasema.... ‘Mpaka tumemaliza show, sasa kwenye muda wa kuondoka nikamwambia Meneja wangu amuite msanii wetu mmoja anaitwa Tausi ili tuondoke, sasa wakati nataka kushuka kwenye gani natembea tu sijui chochote nikashangaa chupa imenipiga usoni, nikadondoka na kubiringika kwenye zile ngazi, kuna mkaka na mdada wakaniona wakanisaidia’

Kajala...‘Aliyenipiga na hiyo chupa ni Mwanaume, simjui na wala sijawahi kumuona hata mara moja…. amekamatwa yuko Osterbay Polisi, nilivyotoka Maisha Club nilipelekwa Hospitali Mwananyamala nimeshonwa usoni aliponiumiza, tukarudi Polisi nikaandika maelezo;

Kwenye sentensi nyingine Kajala amesema ‘Huyu Mwanaume aliulizwa pale Polisi anasema eti ni Pombe, lakini mtu eti Pombe umeingizwa ndani saa moja tu unakumbuka kwamba ni pombe ndio imekufanya hivyo? sio kweli….. itakua tu alidhamiria yeye mwenyewe’

Next PostNewer Post Previous PostOlder Post Home

0 comments:

Post a Comment