Kajala: Simruhusu Mwanangu Awe na Simu

Leave a Comment
Staa wa Sinema za Kibongo, Kajala Masanja amesema hawezi kumruhusu binti yake Paula kumiliki simu ya mkoni kwasasa.

Akiongea kwenye kipindi cha The Sporah Show hivi karibuni, Kajala alisema anaweza kufikiria kumruhusu kuwa na simu hadi pale atakapomaliza kidato cha nne.

Kajala alisema mtoto wake pia hayupo kwenye mtandao picha wa Instagram.
“Paula hana simu kabisa, sio tu simu ya Instagram hata tu kitochi, hana simu,” alisema.
“Na hawezi kuwa na simu labda mpaka afike form four, yaani nitakayomnunulia mimi,”Kajala alisisistiza.

Hongera sana Kajala kwa msimamo wako,simu ni chanzo cha maovu mengi kwa mabinti wa shule

chanzo:Bongo5
Next PostNewer Post Previous PostOlder Post Home

0 comments:

Post a Comment